Thursday, July 10, 2014

JUSTIN BIEBER SASA KULIPA FAINI YA DOLA 80,900 KWA KUMRUSHIA MAYAI JIRANI YAKE


STAA wa muziki wa Pop, Justin Bieber atalipa faini ya dola 80,900, kuhudhuria kozi ya wiki 12 kudhibiti hasira zake na siku tano za kushiriki kazi za kijamii kwa kosa la kumrushia mayai jirani yake.

Staa huyo pia atatakiwa kukaa umbali wa yadi 100 kutoka kwa familia hiyo huku akiwa chini ya uangalizi kwa muda wa miaka miwili.

Bieber alinaswa na jirani yake akirusha mayai katika nyumba yake mwezi Januari na hukumu yake imetoewa jana huko Los Angeles na kuhudhuriwa na mwanasheria wake, Shawn Holley.

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top