Thursday, July 3, 2014

ALIYEMTESA HAUSIGELI SIKU 730 NAYE AHENYESHWA VIKALI.

Hausigeli aliyedaiwa kuteswa na mtuhumiwa huyo

 Mwanamke Yasinta Rwechengura, mkazi wa Boko wilayani Kinondoni, Dar anayekabiliwa na kesi ya kutuhumiwa kumtesa hausigeli wake kwa miaka miwili (siku 730), amejikuta akihenyeshwa mahakamani.Hayo yamemkuta juzi alipofikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Kinondoni kujibu tuhuma zinazomkabili ambapo alikuwa akipokea amri kutoka kwa askari na kumfanya kukosa raha.

Mtuhumiwa akiwa chini ya ulinzi.

Msala huo unagusa hisia za wengi ndiyo maana watu kutoka viunga mbalimbali vya Jiji la Dar walifurika mahakamani hapo kusikiliza mwenendo wa kesi hiyo iliyosomwa mbele ya Hakimu Mkazi, Boniphace Lihamwike.

Akisoma kesi hiyo mahakamani hapo, wakili wa serikali ambaye alikuwa  upande  wa jamhuri, Mohamed Salum alisema anaiomba mahakama hiyo kutotoa dhamana kwa  mtuhumiwa kwa sababu za kiusalama.

Sababu ya pili alisema bado hali ya mgonjwa ni mbaya na amelazwa kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Akipelekwa mahabusu.

Kesi hiyo ambayo inafuatiliwa kwa ukaribu na wanaharakati wa haki za  binadamu, awali ilikuwa inasikilizwa na Hakimu Suleiman Mzava ambaye juzi hakufika mahakamani hapo  kutokana na uhamisho alioupata na badala yake  kesi hiyo ilitajwa kwa Hakimu Lihamwike.Upande unaomtetea mtuhumiwa huyo uliokuwa ukiongozwa na wakili wa kujitegemea, Msomi Gidion, uliiomba mahakama kumpa mteja wao dhamana lakini ukagonga mwamba.
Hata hivyo, wakili Mohamed aliendelea kuiomba mahakama kwa mara nyingine kutotoa dhamana kwa  mtuhumiwa kwa sababu alizozitoa awali.

Wananchi wakimshangaa

Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, alisema pande zote zilikuwa na hoja akianza na upande wa mtuhumiwa ambapo alitoa ufafanuzi kuwa ni haki  yake ya kikatiba kupata dhamana lakini upande wa jamhuri nao ulikuwa na hoja.

Hakimu huyo alisema kuwa shauri hilo  kwa mara ya kwanza lilianzia kwa hakimu mwingine na ndani ya faili la kesi hiyo hakukuwa na vielelezo vyovyote hivyo kuirudisha kesi hiyo kwa hakimu kiongozi kwa ajili ya kupangiwa hakimu atakayeisikiliza.

Baada ya hapo, mtuhumiwa alipandishwa kwenye karandinga na kurudishwa mahabusu kwenye Gereza la Segerea, Dar kuendelea kuhenya hadi atakapopata dhamana huku wananchi waliofika mahakamani hapo wakimshangaa.

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top