Saturday, June 14, 2014

Rais Obama anaangalia uwezekano wa kupeleka tena jeshi Iraq kukabiliana na mashambulizi ya wanamgambo wa kiislam.


Rais Obama amesema anaangalia uwezekano wa kuisaidia Iraq kukabiliana na mashambulizi ya wanamgambo wa kiislam waonadhibiti eneo kubwa la kaskazini mwa Iraq .
Hata hivyo maafisa wa Marekani wamesema wanaendelea na majadiliano ili kuona kama wanaweza kutuma vikosi vya kijeshi katika kukabiliana na kundi hilo.

Nchini Iraq kwenyewe wanamgambo hao wamepata udhibiti zaidi mashariki mwa jimbo la Diyala, lakini mashambulizi ya anga ya vikosi vya serikali yameelekezwa magharibi zaidi eneo la Samara.
Katibu wa NATO Anders Fogh Rasmussen amesema hali hiyo haivumiliki juu ya vitendo dhidi ya wanamgambo hao wa kiislam japo kuwa Iraq yenyewe inapaswa kutafuta namna ya kutatua mgogoro huo.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani Jen Psaki ametoa ufafanuzi akidai kuwa watalaam wao bado wanaendelea na majadiliano na kwamba si nia ya nchi yake kurejesha vikosi vyake Iraq japo kuwa inaona haja ya kutoa msaada kwa nchi hiyo kutokomeza makundi hayo

Ungependa stori kama hizi zisikupite na zikufikie wakati wowote? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza Like hapo juu

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top