STAA wa muziki Bongo, Isabela Mpanda ‘Bela’, amefunguka kuwa amekuwa akikabwa usiku kishirikina na msichana wake wa kazi aliyemtoa mkoani Mtwara.Akielezea tukio hilo, Bela alisema mara baada ya kumleta mjini binti huyo, alikuwa akimtokea mara kwa mara ndotoni akitaka kumyonga na alipomuuliza alikiri kuwa yeye amerithishwa mikoba ya kichawi na bibi yake.
“Daah! Ilikuwa kivumbi mwenzangu ndani hakukaliki, nimeamua kumrudisha kwao Mtwara maana nilikuwa silali vizuri,” alisema Bela.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment