MWIGIZAJI
wa kike wa filamu Kibongo Husna Chobis ‘Awena’ amesema kuwa baada ya
kurudi katika biashara zake nje ya nchi yupo tayari kuolewa lakini kwa
mwanaume mwenye fedha za kutosha na siyo mbabaishaji.
Akifafanua zaidi, msanii huyo amesema hawezi kuolewa na mwanaume ambaye hawezi hata kumiliki Bajaji.
Pia, amedai kwamba mwanaume mwenye fedha za kubadilisha mboga hana mpango nao.
“Kuzaliwa katika familia ya kimaskini ni bahati mbaya, lakini kuchagua mume maskini ni uzembe na hustahili kusamehewa,” alisema.
Aidha aliongeza kuwa kutembea kwake amejifunza mambo mengi na kuona mastaa wa Ulaya huwa wanaolewa kwa maslahi.
Mwigizaji
huyo aliyejizolea umaarufu katika Filamu ya Ndase, alisema moja ya
matatizo ya ndoa za Kitanzania au Kiafrika ni kukosea katika uchaguzi na
kuingia katika uhusiano.
Ungependa stori kama hizi zisikupite na zikufikie wakati wowote? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza Like hapo juu
“Wengi huishia kupotezeana muda kisha kutengana kutokana na kuwa uzembe wa kukosea katika uchaguzi wa mume au mke,” alisema.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment