Wednesday, June 25, 2014

MACHANGU WAMVAA CHOKI KWENYE SHOO NA KUMFANYIA MAMBO YA KHANGA MOKO.


Staa wa Bongo Dansi, Ally Choki ‘Mzee wa Farasi’ akiimba pamoja na madada hao.

 KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, wadada wa mjini waliodaiwa kuwa machangu walimpa wakati mgumu, staa wa Bongo Dansi, Ally Choki ‘Mzee wa Farasi’ baada ya kumvamia jukwaani na kumfanyia mambo ya hovyo.
Tukio hilo lililoshobokewa na wanaume wakware, lilitokea wikiendi iliyopita katika Ukumbi wa Meeda, Sinza – Mori, Dar ambapo mkali huyo aliye Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’ alikuwa akiporomosha shoo ya nguvu na kundi lake

Muziki ulipokolea wadada hao waliokuwa wamevalia nguo saresare walikwenda jukwaani na kuanza kucheza kabla ya baadaye kuanza kujiachia kihasarahasara.

Madada hao wakicheza kwa furaha.

“Mh! Hawa wadada vipi? Mbona wanaleta mambo ya Kanga Moko hapa? Cheza gani ile ya aibu namna ile...hawa lazima ni machangu. Wamekosa wateja sasa wamekuja kumtega Choki, maana mambo yale kama siyo machangu utawaitaje?” alisikika dada mmoja akisema ukumbini humo.

Lakini hali ilikuwa tofauti kwa wanaume wakware ambao kwao ilikuwa faraja kujionea mambo ya chumbani hadharani, kwani walikuwa wakiwashangilia.

Hata hivyo, wakati wadada hao wakiendelea kufanya yao, Choki wa watu hakuwa na la kufanya, zaidi ya kuduwaa na kuwashangaa tu.

Madada hao wakilisakata rhumba pamoja na wapenzi wa bendi hiyo.

Ili kuonyesha kuwa vichwani mwao hamnazo, wadada hao hawakuona haya kuachia maungo yao wazi, hata pale makufuli yalipobaki nje,  walionekana hawana habari kabisa.

Ilifikia mahali, mmoja wao akaenda mbali zaidi baada ya kutaka kuvua nguo, hakupewa nafasi hiyo, mabaunsa walimbeba na kumtoa ili wastaarabu waendelee kuburudika na Wazee wa Kizigo.


Ungependa stori kama hizi zisikupite na zikufikie wakati wowote? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza Like hapo juu

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top