MAJANGA! Staa wa filamu na muziki Bongo, Isabela Mpanda alijikuta akichezea kipigo kutoka kwa mke wa kigogo mmoja maarufu jijini Dar baada kutuhumiwa kuwa anaiba penzi la bosi huyo.
Taarifa zinasema baada ya kuchezea kipigo hicho, Isabela alikiri kutenda kosa hilo pasipo kujua yule jamaa alikuwa ni mume wa mtu.
Alipotafutwa Isabela, alisema anakumbuka tukio hilo ambalo lilimfanya tangu siku hiyo aogope kabisa waume wa watu.
“Daah! We acha tu tangu siku hiyo nilikuwa makini sana na waume wa watu maana nilipigwa pasipo kuwa na kosa,” alisema Isabela.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment