Thursday, June 19, 2014

HOFU YA BOMU YATANDA MLIMANI CITY.

Eneo la Mlimani City.
HUKU watu karibia 60 nchini kenya wakiuawa kwenye mashambulizi ya kigaidi, katika hali isiyo ya kawaida nchini Tanzania, walinzi wa Maduka ya Mlimani City jijini Dar wamejikuta wakipata mchecheto wa aina yake baada ya kitu kilichodhaniwa ni bomu kukutwa kwenye eneo la kuegeshea magari.

Walinzi wa maduka ya Mlimani City jijini Dar wakikagua kitu kinachosadikika kuwa ni bomu.

Tukio hilo lilitokea Juni 16, mwaka huu ambapo kwa mujibu wa shuhuda aliyeomba kusitiriwa jina, aliona gari dogo jeupe likiangusha kifaa hicho kilichodhaniwa ni bomu kisha likatoweka.
Chanzo hicho kilizidi kudai kuwa baada ya gari kutoweka, dada mmoja alipita eneo hilo na kukuta kitu hicho kilichofungwa nyaya kikiwa ndani ya mfuko, akashtuka na kwenda kumtonya mlinzi wa eneo hilo ambaye alifika mara moja na kuwaita wenzake.

...Ukaguzi ukiendelea.

Taarifa za uwepo wa kifaa hicho ziliwafikia waandishi wetu waliokuwa wakipiga doria katika eneo hilo na haraka wakasogea karibu kuwashuhudia walinzi hao wa Kampuni ya Ulinzi ya Omega wakiwa wamekizunguka kifaa hicho kwa umakini mkubwa.

Walinzi hao walimuita kiongozi wao ambaye alifika na kukichunguza kifaa hicho ambapo alipokifungua aligundua ni betri bovu la pikipiki.Waliichukua betri hiyo na kuitupa huku wakitawanyika kurudi kwenye maeneo yao ya ulinzi.

Maoni ya Mhariri
Kutokana na kuwepo kwa matukio ya kigaidi yaliyotokea nchini  Kenya hivi  karibuni, ni vyema jeshi la polisi likawa na tahadhari katika maeneo yanayokusanya watu wengi kama Mlimani City.

Ungependa stori kama hizi zisikupite na zikufikie wakati wowote? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza Like hapo juu

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top