Monday, June 16, 2014

48 WAFA PAPO HAPO KATIKA SHAMBULIO HUKO LAMU NCHINI KENYA JANA USIKU.


Daladala zilizochomwa moto wakati wa shambulio hilo la Mpeketoni, Lamu nchini Kenya.

Magari yaliyochomwa moto katika kituo cha polisi cha Mpeketoni.

WATU zaidi ya 48 wameuawa, hoteli mbili, kituo cha polisi na kituo cha mafuta kuchomwa moto baada ya shambulio lililotokea eneo la Mpeketoni, Lamu nchini Kenya jana usiku.

Kituo cha Polisi cha Mpeketoni, hoteli ya Breeze View na Taweel ndivyo vilivyochomwa moto na moshi ulikuwa bado unafuka asubuhi hii.

Imeelezwa kuwa washambuliaji walitokomea na silaha na magari ya polisi kutoka kutuo hicho cha polisi baada ya kushambulia.

Awali washambuliaji hao waliteka daladala mbili 'matatu' eneo la Witu kabla ya kufanya shambulio hilo.

Wananchi walikimbilia katika nyumba zao wakati polisi wakijibizana risasi na magaidi hao ambapo mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo anadai kusikia washambuliaji hao wakisema "ambieni baba yenu atoe jeshi Somalia” wakimaanisha wamwambie Rais Kenyatta aondoe jeshi nchini Somalia.

Makundi ya Al Shabaab na MRC militia yanadaiwa kuhusika na shambulio hilo

Ungependa stori kama hizi zisikupite na zikufikie wakati wowote? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza Like hapo juu

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top