Sunday, April 6, 2014

Kama huamini nenda ukashuhudie; Chungu chenye maini chaibuka juu ya kaburi huko Iringa.


 

Hapa ndipo chungu hicho kilipoibukia

Hivi ndivyo vilivyokuwemo ndani na damu ,maini na kichwa cha ndege

Hapa msamaria mwema akionyesha vitu vilivyopo ndani

Mzee Mlawa akiwasha kiberiti kwa ajili ya kuteketeza ushirikiana huo

Tunguli ikiteketezwa kwa moto

Wananchi na mzee Mlawa kulia wakitazama tunguli hilo likiteketea kwa moto

MAUZA uza matupu kaburi la mtoto Agnes Mlawa (8) mkazi wa Ilala katika Manispaa ya Iringa aliyezikwa mwaka jana na leo baba wa mtoto huyo kakuta chungu cha ajabu chenye damu,maini na kichwa cha ndege kimechimbiwa kaburini.

Tukio hilo la aina yake limetokea leo majira ya saa 2 asubuhi katika makaburi ya Makanyagio mjini Iringa wakati baba mzazi wa mtoto huyo Bw. Mlawa wakati akichembua kaburi hilo na mara baada ya kumaliza ghafla alishuhudia tukio hilo la chungu cha ajabu kuibuga juu ya kaburi hilo .


" mimi hapa leo nilikuja kusembua kaburi la mwanangu ila baada ya kumaliza ghafla nilikuta kama damu zinaruka juu kutoka kaburini na baada ya kuchunguza ndipo nilipoona chungu hicho kikiibuka huu ya kaburi "

Alisema kuwa chungu hicho kilikuwa kimefungukwa na kitambaa cheusi juu ambacho kimelowa dawa na kufungwa kamba ya nguo ya kijani na kutokana na tukio hilo la ajabu alilazimika kuacha jembe juu ya kaburi na kukimbia kuita watu wanaopita barabarani ili kuomba msaada zaidi.

Mzazi huyo anadai kuwa mazingira ya kifo cha mtoto wake yalikuwa ni ya kushangaza baada ya kuugua kwa muda wa siku nne pekee na kufariki dunia .

Hata hivyo alisema kwa kuwa kwa upande wake haamini mambo ya kishirikiana hakuona sababu ya kumwita mganga wa kienyeji kwa ajili ya kushughulikia kuchoma chungu hicho na badala yake kuamua kuifanya kazi hiyo mwenyewe hasa akiamini nguvu ya Mungu zaidi.

" Napenda kuwashukuru wananchi waliofika hapa kwa kunitia nguvu na pia kuwashukuru madereva boda boda akiwemo kijana Ahmed kwa kujitolea mafuta ya Petrol kwa ajili ya kukichoma chungu hiki " Mbali ya mzazi huyo kujitolea kuchuma chungu hicho na kuteketeza vitu vilivyo kuwemo ndani wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo walilazimika kutimua mbio kuhofu zoezi hilo la uchomaji wa tunguli hizo.
Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top