Wednesday, April 16, 2014

Jeshi la Polisi limetangaza zawadi ya Tsh.Million 10 kwa mtu atakayewezesha kupatikana kwa wahusika wa mlipuko wa bomu Arusha.

Jeshi la Polisi Tanzania limetangaza zawadi ya Tsh.Milion 10 kwa mtu atakayewezesha kupatikana kwa wahusika walioshiriki mlipuko wa bomu lililolipuka Arusha,Bomu hilo lililipuka mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye bar ya Arusha Night Park ambalo lilisababisha majeruhi kadhaa.

Mkurugenzi wa makosa ya jinai Tanzania Dci Isaya Mgula amesema uchunguzi wa awali uliofanywa na wataalam wa mabomu kutoka Jwtz na Jeshi la Polisi Tanzania umebaini bomu hilo limetengenezwa kienyeji mbali na hilo lililolipuka Jeshi la Polisi pia lilibaini bomu lingine lililokuwa kwenye mkoba uliokua umeeegeshwa pembeni ya kiti kwenye bar jirani ya Washington.
Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top