Monday, March 24, 2014

Pigo jingine kwa CHADEMA, Mwenyekiti wa vijana na vijana 100 wilayani Arumeru wahamia CCM.

 picha ikionyesha baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na CCM, wapewa kadi mpya za CCM, katikati ni aliyekuwa Mwenyekiti  wa Vijana CHADEMA kata ya Orturumenti Thomasi Kivuyo.

 Mwenyekiti wa vijana chadema kata ya Orturumenti akiwa anatoa mkono kwa katibu wa siasa uenezi Jonasi Kitoro mara baada ya kukabidhiwa kadi ya ccm


 katibu wa vijana wilaya ya arumeru  akiwa Boniface Mungaya akionyesha baadhi ya kadi zilizorudishwa na wanachama wa chadema.

Jumla ya wananchi 100 wa kata ya Ortumunti  wilayani Arumeru  kutoka katika vyama mbalimbali vya upinzani  wamehamia chama cha Mapinduzi akiwemo mwenyekiti wa   vijana wa  CHADEMA wa kata hiyo .
tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki,wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM,uliofanyika katika kijiji cha Elikiushing kilichopo wilayani Arumeru mkoani hapa.


Akiongea wakati wa kurudisha  kadi ya CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya CCM,Mwenyekiti wa vijana wa CHADEMA, Thomasi Molel alisema kuwa   ameamua kuchukuwa hatua hiyo mara baada ya kubaini kuwa tangu awe mfuasi wa cha hicho (CHADEMA),Hajapata faida yoyote wala hajaona kitu ambacho wananchi wanafaidika kupitia chama hicho.

Alisema kuwa yeye ni mwanasiasa mzoefu kwani alianza kuingia katika siasa tangu mwaka 1995 na anajua siasa vilivyo, hivyo ameamua kuondoka katika chama hicho kwani CHADEMA  ni chama ambacho hakina demokrasia ya kweli  ambayo inatakiwa iwenacho kama chama

Alisema kuwa viongozi wengi wa CHADEMA wamekuwa wanatoa ahadi za uongo kwa wananchi  na mbali ya hivyo pia chama hicho kimekuwa na wasemaji wengi kwani kila kiongozi amekuwa anasema anachotaka badala ya kuwa na msemaji mmoja ambaye ndie atakaeweza kukisemea chama  .

Aidha alibainisha kuwa katika kata yao  tangu upinzani wameingia madarakani hamna kitu ambacho wamewafanyia wananchi badala yake wamekuwa wakiwachangisha wananchi hela nyingi  bila kufanya maendeleo yeyote akitolea mfano mchongo wa shilingi elfu mbili ambao ulichangishwa kwa kila mwananchi wa kike na kiume ikisemekana ela hiyo ingeweza kujengea shule lakini adi leo hela hile aijafanya chochote na aijulikani ilipopelekwa

Aliongeza kuwa kingine ni kile kitendo cha kutosomewa mapato na matumizi  ya kata yao tofauti na kipindi ambacho ccm ilikuwa madarakani hivyo.

Kwa upande wake  katibu wa ccm wilaya ya Arumeru Godfrey Sabuni alisema kuwa  wao kama ccm wanawaapokea wananchama hao na pia wamesikia baadhi ya matatizo yao likiwemo la kutosomewa bajeti ya mapato na matumizi kwa kipindi kirefu na aliwaaidi kufuatilia swala hili kwa kwenda katika ofisi ya mkurugenzi  kufuatilia swala hili.


Aliwasihi wananchi kutofanya makosa katika kipindi hichi kunakoelekea uchaguzi mdogo wa viongozi wa vijiji na vitongoji kwani wakifanya kosa kwa kuchagua viongozi wabovu wataendelea kuteseka  na kata yao haitapata viongozi wazuri.
Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top