Mtela Mwampamba kutoka UVCCM makao makuu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kwakirumbi.
Hii ndiyo hali halisi msafara wa viongozi hao ukielekea kijiji cha Kirumbi kwa ajili ya mkutano wa kampeni kijijini hapo.
Ridhiwani Kikwete anaaminiwa sana chalinze kuwa anaweza kuwatatulia matatizo yao mbalimbali yanayowakabili katika kata yao kwani Ridhiwani Kikwete ni msomi, mwanasheria na mtu aliyepewa dhamana na chama cha Mapinduzi chenye uongozi kuanzia shina mpaka ngazi ya kitaifa hivyo wanao uwezo wa kumpata mahali popote kwani anao udhamini wa kuaminika. hata hivyo tatizo kubwa la kata ya Kibindu ni miundo mbinu ya barabara na maji jambo ambalo wananchi hao wanaeleza kwamba ni muhimu mbunge wao anayekuja aanze nalo, Mbunge aliyepita Marehemu Said Ramadhan Bwanamdogo aliugua muda mrefu jambo lililopelekea wananchi hao kukosa mwakilishi wao katika mambo mbalimbali ya maendeleo jimboni humo.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni kijiji cha Kwamsanja. Wananchi wakiserebuka na muziki kjijini Kwakirumbi kabla ya kuanza kwa mkutano huo. Mtela Mwampamba kutoka UVCCM makao makuu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kwakirumbi. Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Joseph Msukuma akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kwakirumbi.

Ukaguzi wa barabara ukifanyika kabla ya kupita.


Juhudi zikifanyika kunasua gari lililokwama. Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita akipita na gari lake katika madimbwi. Wananchi wakserebeka na muziki kabla ya kuanza kwa mkutano wa kampeni katika kijiji cha Mjembe.

Baadhi ya morani wakifurahia jambo katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye kijiji cha Mjembe kata ya Kibindu.

Safari kuelekea kwenye magari baada ya kampeni kwisha.
(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KIBINDU-CHALINZE)
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment