Friday, March 28, 2014

HAMISA MABETO aelezea utaalamu wake wa kucheza na nyoka.


 MREMBO aliyeng’ara kwenye Shindano la Miss Tanzania mwaka 2011, Hamisa Hassan ‘Mabeto’ amefunguka kuwa, licha ya baadhi ya wasichana wenzake kutokuwa na ujasiri wa kucheza na nyoka, yeye anao.

Mrembo aliyeng’ara kwenye Shindano la Miss Tanzania mwaka 2011, Hamisa Hassan ‘Mabeto’
Akipiga stori na Ijumaa, Mabeto alisema awali alikuwa muoga lakini taratibu alianza kumzoea kiumbe huyo na sasa humtumia hata katika shughuli zake za kimodo anazofanya.
“Hizo picha nilikuwa kwenye ‘photo shooting’ (upigaji wa picha) ila kiukweli nina utaalam wa kucheza na nyoka, unajua siyo kila mtu anao ujasiri wa kumchezea, kwanza anatisha ila mimi nilianza kumzoea taratibu,” alisema Mabeto.
Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top