Friday, March 28, 2014

DIAMOND awaboa waislamu kwa kutupia swaga za staili ya Ngololo kwenye shughuli ya Maulidi.

KIJOGOO wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewachefua waumini wenzake wa
Kiislamu baada ya kutupia swaga za staili ya Ngololo kwenye shughuli ya Maulidi.
Kijogoo wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz akicheza staili ya Ngololo kwenye kaswida.
Tukio hilo lililowagusa waumini hao lilitokea juzikati ambapo kulifanyika Maulidi ya kumtoa nje mtoto wa dansa wake aitwaye Moze Lyobo maeneo ya Mbagala, jijini Dar.

Awali watu waliokuwepo eneo hilo walifurahia uwepo wake lakini kadiri walivyoaanza kugundua kasoro ndipo mambo yalipoanza kuharibika.
Diamond akiwa na mtoto wa Moze Lyobo aliyefanyiwa Maulidi.
“Watu hawakumshtukia, lakini walipomkagua kwa makini na kugundua licha ya kuvaa mavazi ya
Kiislamu ndani yake ana macheni ya dhahabu shingoni kitu ambacho dini hairuhusu,” kilidai
hanzo baada ya mwandishi wetu kufika eneo la tukio na kukuta shughuli imeisha.
Kama hiyo haitoshi, ikaelezwa kuwa Diamond alizidi kuchafua hali ya hewa baada ya kucheza
staili ya Ngololo kwenye kaswida kitu ambacho kiliwashangaza wengi.




“Mwanzo alianza vizuri lakini kadiri dufu lilivyokuwa linakolea, akawa anajisahau na kucheza
Ngololo, kimsingi aliwaboa baadhi ya Waislamu waliokuwa pale,” alisema shuhuda wetu.

Hata hivyo paparazi wetu alitonywa kuwa, baada ya kucheza sana, Diamond alichoka huku jasho
likimchuruzika ambapo aliamua kupumzika na kuwaacha wengine wakiendelea.
Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top