Sunday, March 23, 2014

Breaking news!! Watu wawili wauawa kanisani huko Kenya.



Baadhi ya waumini wa Kanisa la Joy Jesus wakiwa nje ya kanisa baada ya shambulio hilo.
WATU wawili wameuawa wakati wengine kumi wakijeruhiwa baada ya mtu mmoja aliyejihami kwa bunduki kuwafyatulia risasi ndani ya kanisa la Joy Jesus huko Lokoni, karibu na Mombasa nchini Kenya.


Maafisa wa polisi katika wilaya ya Likoni iliyopo kusini mwa Mombasa wamesema kuwa jambazi huyo alilivamia kanisa hilo na kuanza kuwafyatulia risasi waumini hao kiholela.

Bado haijafahamika kama muuaji huyo ana uhusiano na vikundi vya kigaidi au la.
Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top