Sunday, February 2, 2014

Fuatilia jinsi sherehe za Miaka 37 YA CCM inavyofanyika leo jijini Mbeya.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akiongoza matembezi ya mshikamano kutoka viwanja vya Soweto Kwenda Bustani ya Jiji jijini Mbeya huku akiwa amewashikilia watoto wakati wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi CCM yanayofanyika leo mkoani Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine Kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM bara na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Mwigulu Nchema, Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Mzee Philip Mangula na kutoka kushoto ni Katibu wa NEC Fedha na Uchumi Mama Zakhia Megji, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Godfrey Zambi wakishiriki matembezi hayo, Matembezi hayo ya kilomita tano yalianza Saa moja na nusu na kumalizika Saa mbili na robo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MBEYA).

 

 

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akiwasili eneo la Soweto Mwanjelwa jijini Mbeya tayari kwa kuanza matembezi ya mshikamano kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 37 ya CCM

 
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete kulia ,Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Godfrey Zambi na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakisonga mbele.

 
Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe akizungumza na wananchi, kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi. 
 

  
  
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akizungumza na wana Mbeya mara baada ya kupokea matembezi hayo kwenye bustani ya Jiji jijini Mbeya ikiwa ni maadhimisho ya miaka 37 ya Chama cha Mapinduzi yanayofanyika kwenye uwanja wa Sokoine leo jijini Mbeya.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

Share this article

3 comments:

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top