Rais Yoweri Museveni wa Uganda amekataa kuidhinisha muswada wa kupiga marufuku ndoa za watu wenye jinsia moja katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Kama ungeidhinishwa muswada huo ungetoa adhabu kali kwa watu wanaojihusisha na ngono za jinsia moja. Rais Museveni amemuandikia barua Spika wa Bunge, Rebecca Kadaga na kumkosoa kwa hatua ya kupitisha muswada huo Disemba mwaka jana bila ya kuwa na idadi ya kutosha ya Wabunge.
Aidha Rais Museveni amedai kuwa, watu wanaojihusisha na ndoa za jinsia moja wana akili timamu na wanaweza kuokolewa kutokana na tabia hiyo badala ya kuuawa au kufungwa jela.
Mswada huo unatoa adhabu kali kwa watu watakaopatikana na hatia ya kufanya liwati na usagaji ikiwemo ya kufungwa jela maisha. Muswada huo pia unaeleza kuwa, mtu yeyote aliyekuwa na taarifa za watu wanaoshiriki ngono za watu wa jinsia moja na kushindwa kutoa taarifa hizo kwenye vyombo husika atafungwa jela maisha.
Kwa mujibu wa gazeti la Monitor, Rais Museveni amesema kwamba, licha ya kuwashauri wabunge kusubiri hadi serikali itakapoutathmini lakini muswada huo ulishinikizwa zaidi na kupasishwa.


0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment