Tuesday, January 21, 2014

Mwanamke aliyejifungua watoto wanne kwa mkupuo Mbeya apata msaada.Wadai nanyi saidieni basi.

 

Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Vanessa (kushoto) iliyopo Isyesye Jijini Mbeya, Shukrani Gidion akimkabidhi Godoro Aida Nakawala mama aliyejifunguwa watoto wanne

Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Vanessa iliyopo Isyesye Jijini Mbeya, Shukrani Gidion, amempa msaada wa vitu mbali mbali Mwanamke Aida Nakawala(25)aliyejifungua watoto wanne kwa mkupuo.


 Akizungumza katika hafla ya kumkabidhi msaada huo iliyofanyika katika Wadi la wazazi katika Hospitali ya Wazazi Meta anakoendelea na matibabu, Mkurugenzi huyo alisema ni jambo la kushangaza kwa binti mdogo kupata watoto wengi katika njia ya kawaida.

Alisema katika maisha yake ameishia kusikia mapacha wawili au watatu lakini Mapacha Wanne imemshangaza sana jambo lililomgusa kumsaidia baadhi ya vitu kulingana na mahitaji ya Mama Wanne ambaye hata hivyo hali yake inaendelea vizuri pamoja na watoto wake.
Vitu alivyotoa ni pamoja na Godoro la futi Tano kwa ajili ya malazi ya watoto baada ya kuruhusiwa kutoka Hospitali, Blanketi, Shuka, Chandarua, Nguo za Mama, Mataulo ya Watoto pamoja na nguo zake,Vifaa vya kunyonyeshea pamoja na Maziwa ya Watoto(lactojeni) ambavyo jumla yake vikigharimu zaidi ya Shilingi Laki tano.
CHANZO MBEYA YETU

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top