Sunday, January 19, 2014

Mtangazaji wa BBC alifahamika kwa kutangaza kipindi cha BBC Focus on Africa Komla Dumor amefariki Dunia

Mtangazaji wa BBC kwenye picha hapo juu amefariki dunia akiwa nyumbani mwake London kwa tatizo la moyo.

Mtangazaji huyu  ambaye ni Raia wa Ghana amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 41.
Alikuwa maarufu sana katika kipindi cha BBC focus on Afrika na hili litakuwa pigo kubwa kwani itachukua mda kumweka mtu mwingine sehemu yake kwani yeye alikuwa anafiti sana.

Alijiunga na BBC mwaka 2007 akipewa kazi ya kutangaza kwenye redio kabla baadaye kuanza kutangaza kwenye television.Komla Dumor pia aliingia katika African Magazinekwenye  listi ya watu 100 maarufu zaidi Afrika.
Komla Dumor alizaliwa tarehe 3 October 1972 katika mji wa Accra, Ghana.

Alisoma BA in Sociology and Psychology kutoka University of Ghana, na Masters in Public Administration kutoka Harvard University. 

Pia mwaka 2009 alikuwa mwafrika wa kwanza kutangaza Komla katika taarifa ya habari kwa habari za biashara yaani Business Report on BBC World News.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top