Saturday, January 18, 2014

Mke wa Mtu anaswa Guest Live akipigwa Mambo; Soma ujue mabo Gani;

 Bonge akiwa kitandani kauchapa usingizi chumbani huku kitandani kukiwa na kondomu kibao.
Makubwa madogo yana nafuu! Kwenye kamatakamata na fumuafumua ya magenge ya biashara haramu ya ngono mjini hapa imemkumba bonge la jimama ambalo lilinaswa gesti likisubiri mteja.


Tukio hilo lilijiri hivi karibuni wakati vijana wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ilipopata mwaliko maalum kutoka jeshi la polisi Moro kwa ajili ya kufichua biashara hiyo haramu ambapo mwanamke huyo alinaswa kauchapa usingizi chumbani huku kitandani kukiwa na kondomu kibao.

Ndani ya gesti maarufu ya Itigi iliyopo maeneo ya Msamvu, inayotumiwa zaidi na madereva wa malori ya masafa marefu ndipo alipobambwa bonge ambaye katika utetezi wake alidai kuwa ni mke wa mtu.
“Naombeni mnisamehe nilikuwa najitafutia riziki, baba J akijua ataniua jamani amesafiri, akirudi nimekwisha,” alisema kwa aibu mwanamke huyo. aliyejulikana kwa jina la mama J.
Bonge akiwa katika pozi la aibu baada ya kubanwa na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, kitendo hicho kilikuwa cha aibu mno mbele ya jamii.
Hata hivyo, pamoja na utetezi wake, bonge aliunganishwa na wenzake walionaswa kisha akapewa henyahenya na polisi kabla ya kutupwa nyuma ya nondo za mahabusu kusubiri sheria kuchukua mkondo wake.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top