Wednesday, January 22, 2014

Jeshi la Nigeria lapiga marufuku wasaniaa kutumia sare za jeshi kwenye Video zao.


Jeshi la Nigeria limetoa onyo kwa watu wote maarufu wa nchi hiyo kutovaa tena nguo za kijeshi uraiani na hata kwenye video zao kwa upande wa Wasanii kutokana na kulidhalilisha jeshi la nchi hiyo.
Kwenye barua ya wazi iliyoandikwa na jeshi la nchi hiyo, kuna maneno yanasema ‘Ni marufuku kwa yeyote kuonekana na nguo za kijeshi popote, hii ni kwa Watu maarufu na wananchi wengine baada ya kugundulika pia nguo za kijeshi zimekua zikivaliwa kwenye music videos, photo shoots na kwenye matamasha’

 

‘Vivyo hivyo, kwenye videos na photo sessions watu maarufu wa Nigeria kama Jesse Jags wameonekana wakivuta bangi wakati wako ndani ya mavazi ya kijeshi kitu ambacho ni kama kulichafua au kulidhalilisha jeshi, hivyo basi yeyote atakaepatikana na makosa haya hatua tutakazomchukulia hazitaulizwa au kuhojiwa’ Mastaa wengine wa Nigeria ambao hupenda kuvaa nguo za kijeshi ni pamoja na Iyanya, Wizkid, Davido, Tekno Miles, Chidinma


Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top