Thursday, December 11, 2014

LULU AMUWAHI IDRIS; ASEMA ANA URAFIKI NAE.

ACHANA na watu kibao waliojitokeza mitandaoni na kudai wana undugu na mshindi wa Shindano la Bigbrother Hotshot (2014), Idris Sultan (21), mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ ndiye mtu wa kwanza kabisa kujinadi kuwa na urafiki na mshindi huyo aliyejinyakulia zawadi ya shilingi milioni 510.

Mwigizaji wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiwa na Idris.

Idris ambaye alinyakua kitita hicho nchini Afrika Kusini wikiendi iliyopita, aliwasili jana nchini na kupokelewa na Wabongo wengi ambao walimpongeza kutokana na ushindi huo alioupata baada ya kuwagaragaza washiriki saba wa nchi tofauti za Afrika.

Siku alipotangazwa ushindi, kesho yake (Jumatatu) Lulu ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kutupia picha ya zamani katika mtandao wa Instagram akiwa na Idris na kuacha gumzo kwa wafuasi wa mtandao huo juu ya ukaribu huo kiasi cha kupiga picha ya pamoja.

Elizabeth Michael ‘Lulu’ akipozi.

Picha hiyo ilizua gumzo huku kila shabiki akisema lake, kuna ambao walimpongeza kwa kuwa na urafiki na nyota huyo mpya lakini wengine wakaponda.“Jamani tuache ushamba yeye amempongeza tu kama alivyokuwa akifanya tangu zamani, kwani kuna ubaya?” alihoji mdau mmoja.

Mbali na Lulu, baadaye wasanii wengine walifuata mkumbo huo wa kuweka picha wakiwa na Idris ambazo wengi walikuwa na lengo la kumpongeza mshindi huyo ingawa Wabongo wengi walidai kuwa wanajipendekeza.Katika mazungumzo yake na mwanahabari wetu, mbali na mipango mingine, Idris amepanga kuwekeza sehemu ya fedha zake katika soko la filamu Bongo. 

BILIONEA NIGERIA AMZAWADIA TAYO $ 350,000 BAADA YA KUKOSA ZA BIG BROTHER HOTSHOTS.



HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online