Tuesday, December 2, 2014

36 WAUAWA NA AL SHABAB KENYA.

Baadhi ya Wanamgambo wa Al Shabab.

TAKRIBANI watu 36 wanahofiwa kufariki katika shambulio lililotokea kwenye machimbo ya kokoto karibu na mji wa Mandera kaskazini mwa Kenya. Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya limethibitisha.

Wakazi wa eneo hilo wamesema waathirika wote wa tukio hilo ni watu wasio Waislam ambao walikuwa wakifanya kazi katika machimbo hayo yaliyopo Kormey kilomita 15 kutoka mji wa Mandera Kaskazini mwa Kenya.

Tukio hili linafuatia tukio la wiki moja iliyopita ambapo watu wapatao 28 waliuawa katika shambulio la basi la abiria huko Mandera.
Kundi la wapiganaji wa Kiislam la Al Shabab limekiri kuhusika na mauaji hayo.

JISOMEE MWENYEWE HAPA VIZURI NA TARATIBU RIPOT YA TEGETA ESCROW....YOU CAN'T BELIEVE ON Y's EYE HUYU NAE KAPEWA MGAO.


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top