Thursday, November 13, 2014

Roboti yarudisha picha ya kwanza duniani baada ya kutua kwenye kimondo angani; Icheki hapa.

Baada ya safari ya miaka kumi katika anga za juu, chombo cha anga za mbali cha Ulaya kimevuka kilomita chache za mwisho kutoka ardhini kutekeleza kile kitakachokuwa kifaa cha kwanza kuwahi kutengenezwa na binadamu kutua kwenye kimondo.

Roboti hiyo iliyotengezwa Ulaya kwa jina Philae, imefanikiwa kutua katika kimondo likiwa ni jambo la kihistoria kuwahi kushuhudiwa.

Aidha roboti hiyo ilitua katika Kimondo kinachojulikana kama 67P/Churyumov-Gerasimenko saa kumi jioni saa za Ulaya.

Kulikuwa na vifijo na nderemo pamoja na wanasayansi kupigana pambaja katika chumba ambako shughuli hiyo ilikuwa inadhibitiwa mjini Darmtadt, Ujerumani baada ya ishara kuonyesha kuwa roboti hiyo ilikuwa imetua kwenye kimondo.

Ishara ya kuonyesha kuwa roboti hiyo ilifanikiwa kutua ulikuwa mwanga kutoka kwenye roboti hiyo.

"Hii ni hatua kubwa sana katika historia ya binadamu kulingana na wanasayansi hao.
SOURCE; BBC/SWAHILI

Huu si ushabiki ni Ngono zembe; Yaani wanafanya Hivi eti kisa Gor Mahia Kushinda KPL.


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online