Basi la Wibonela wakati likitolewa eneo la tukio.

Wananchi wakishuhudia basi la Wibonela lililopinduka leo asubuhi huko Kahama.
WATU kadhaa wamepoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa asubuhi hii kwenye ajali ya basi la Wibonela lililokuwa likitoka Kahama kwenda Dar lililopinduka eneo la kona ya Phantom, Kahama.
Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi uliopelekea dereva wa basi kushindwa kulimudu lilipofika kwenye kona ya Phantom na kupelekea kuingia mtaroni na kupinduka.
Idadi kamili ya waliopoteza maisha na majeruhi kwenye ajali hiyo bado haijafahamika.
Baadhi ya miili tayari imetolewa katika eneo la ajali huku majeruhi nao wakikimbizwa kwenye Hospitali ya Wilaya Kahama kwa matibabu.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment