Wednesday, October 22, 2014

‘UKAWA’ NYINGINE YAZALIWA BONGO MOVIE.

 WASANII wa filamu ambao hivi karibuni waliripotiwa kujitoa katika kundi la Bongo Movie Unity wamedaiwa kuunda la kwao linalojulikana kama Ukawa ambalo litakuwa chini ya uongozi wa Mwenyekiti aliyetimuliwa, Steven Mengere maarufu kama Steve Nyerere.

Baadhi ya Wasanii wa bongo Movies waliokuwa pamoja katika uongozi kabla ya mzozano.

Baadhi ya wasanii wanaotajwa kuunda kundi hilo kwa mujibu wa chanzo chetu makini ni pamoja na Devotha Mbaga, Salama Salmin ‘Sandra’, Halima Yahya ‘Davina’ na wengineo.

“Yaani sasa hivi haya makundi mawili kuna vita kali sana, kila moja linataka lionekane kwamba lina nguvu kuliko lingine, hata jina la Bongo Movie Unity limebadilishwa sasa hivi linaitwa Bongo Movie Stars,”kilisema chanzo hicho.

Aliyekuwa Katibu msaidizi wa Bongo Movies Unity, Devotha Mbaga.

Mussa Issa ‘Cloud’ alikiri kubadilishwa jina kwa Bongo Movie Unity na pia amesikia habari za kuwepo kwa kundi la Ukawa wakati Steve Nyerere alisisitiza kuwa bado ni mwanachama wa Bongo Movie Unity na kwamba mtu anayetaka kuwagombanisha wasanii anajulikana.

South African athlete Oscar Pistorius jailed for FIVE years for killing Reeva Steenkamp.



HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top