Thursday, October 16, 2014

MAMA KANUMBA AKANUSHA KUTEMBEA NA SERENGETI BOI;


MAMA wa marehemu, Steven Kanumba, Flora Mtegoa amekanusha vilivyo taarifa zilizozagaa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na kijana mdogo ambaye amemzidi umri (serengeti boy).

Mama wa marehemu, Steven Kanumba, Flora Mtegoa (mwenye kipaza sauti) akizungumza jambo.

Mama Kanumba ambaye pia amefuata nyayo za mwanaye kwa kujiingiza katika uigizaji, alifunguka hayo alipokuwa akizungumza na mwanahabari wetu mambo mbalimbali yahusuyo maisha yake binafsi na sanaa kwa jumla.

Lilipofika suala la tuhuma hizo ambazo zimewahi kuripotiwa na baadhi ya magazeti (si ya Globa Publishers Ltd) kwamba anatembea na dogodogo, mzazi huyo alisema taarifa hizo ni za kipuuzi na hazina ukweli wowote.

“Huo ni uongo tu kwa kweli, hakuna kitu kama hicho, mtu mzima kama mimi naanzaje kufanya vitendo kama hivyo? Heshima yangu itakuwa wapi?” alihoji mama Kanumba.

Mama hakusita kutoa ufafanuzi zaidi juu ya madai hayo kwenda mbele hadi kufikia hatua ya kudai kuwa anaonekana na dogodogo huyo katika maeneo tofauti.

“Wanasema nimekuwa nikionekana naye sehemu tofauti? Inawezekana akawa ni huyu mwanangu Hotma Peter ambaye nimekuwa nikishirikiana naye kwenye kazi mbalimbali kwa kuwa watu hawamjui na walizoea kuniona nikiwa na Seth Bosco (mdogo wa marehemu), ukweli sina bwana na wala sihitaji hata awe pedeshee wa aina gani,” alisema mama Kanumba.

ANGALIA PICHA MBALIMBALI ZA SHEREHE YA KUZALIWA MAPACHA WA MENGI.


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online