Monday, October 13, 2014

BWANA HARUSI AINGIA MITINI SIKU YA KUFUNGA NDOA; BIBI HARUSI HALI TETE.



Binti anayetambulika kwa jina moja la  Husna (16)(mwenye shela) , aliyetaka kuolewa na bwanaharusi, Rahim (30).

Aiseee! Ndoa ya binti aliyetambulika kwa jina moja la  Husna (16), imebuma baada ya bwanaharusi, Rahim (30), kuingia mitini muda mfupi kabla ndoa kufungwa.

Tukio hilo la aina yake lilijiri maeneo ya Kitunda-Kati jijini Dar, wiki iliyopita ambapo chanzo makini kiliwajulisha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers kwamba, kuna ndoa ya mtoto inafungwa kinyume cha sheria.

Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, OFM walitinga kwenye sherehe hiyo na kuanza kuwahoji baadhi ya ndugu ambao walikiri kwamba kweli ile ilikuwa ni ndoa ya mtoto aliyeacha shule akiwa kidato cha pili.
Akizungumza na OFM, Husna alisema aliamua kuolewa kwa sababu aliacha shule kutokana na kukosa ada.

Husna akilia baada ya ndoa kubatilika.

Alisema kwamba, darasani alikuwa haelewi chochote alichokuwa akifundishwa hivyo hakuwa na kazi yoyote.“Baba na mama yangu wameachana siku nyingi, sasa nilikuwa nalipiwa ada na mama huku kipato chake kikiwa ni kidogo.

“Niliamua kuachana na shule maana nilikuwa sielewi chochote kwa sababu niliugua mapepo, nimeamua mwenyewe kuolewa jamani maana sina kazi ya kufanya,” alisema Husna.Baada ya baadhi ya watu kuwashtukia OFM, walimpa taarifa bwanaharusi kwa simu na hakuonekana na ndoa hiyo ikaishia hewani kwani jamaa huyo hakufika kwa kuhofia hilo.

Mama akimfariji Husna

Baadhi ya ndugu wa bwanaharusi walikuja juu na kutaka warudishiwe mahari yao lakini mjomba wa mtoto huyo aliwasihi kwamba watakaa kama familia na watazungumza na wako tayari kurudisha mahari.
Baada ya ndoa hiyo kubuma, mtoto Husna aliangua kilio huku akisema kwamba anampenda huyo mchumba’ke huku mama yake naye akiangua kilio akidai anaumia kwani hajui atakapozitoa hizo fedha za mahari shilingi laki nne kwani kipato chake ni kidogo.

Annie Idibia brings village life to the city.


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top