STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper Masawe ‘Jack Wolper’ amejikuta akitumika kwenye utapeli wa mamilioni ya shilingi kupitia mitandao ya kijamii bila yeye kujua,limeinyaka.
Staa wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper Masawe ‘Jack Wolper’
Akizungumzia sakata zima huku alibubujikwa na machozi, Wolper alisema: “Siku moja nilikutana na dereva teksi mmoja aitwaye Ismail, baada ya kupiga stori nilimpa namba yangu ya simu na yeye akanipa yake, tukaagana.

“Siku chache baadaye Ismail akanipigia simu na kuniuliza kulikoni naomba sana watu wanisaidie pesa kwenye WhatsApp kwa ahadi ya kuwarejeshea?“Akaniambia kama nina tatizo bora wakati mwingine nimshirikishe kuliko kila kukicha kuombaomba pesa.

Staa wa filamu, ‘Jack Wolper’ akipozi.
Akaongeza kuwa, baada ya kugundua utapeli huo akashangaa wanajitokeza watu wakisema wanamdai ambapo imebainika mtu huyo alikuwa kakopa pesa kwa watu tofauti zinazofikia shilingi milioni 10 lakini wengi walimuelewa hivyo kuripoti tukio hilo kwa vyombo vinavyohusika ili kumsaka mtuhumiwa.
BAADA YA KUMWAGANA NA MFANYABIASHARA WA MADINI; LULU AMNASA MENEJA WA WEMA SEPETU.
TAHADHARI YA MHARIRIBaadhi ya watu wamekuwa wakitapeli kupitia njia ya mtandao hivyo ni vyema kila mmoja kuwa makini ili kuepukana na matatizo kama yaliyomkuta Wolper.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment