Tuesday, September 9, 2014

SINTA ATOA YAKE BAADA YA SHILOLE KUTISHIA KUMPIGA POPOTE ATAKAPOMUONA.

Msanii wa muziki na maigizo nchini Shilole kulia na mumewe ambae ametangaza kumvulumushia makonde mazito Sintah popote atakapomuona.

Msanii mkongwe kwenye tasnia ya afrika na kati Sintah amefunguka kuhusu vitisho anavyopewa na msanii mwenzake wa muziki na maigizo Shilole kuwa ajiandae kuchezea kipigo cha mbwa mwizi popote atakapomuona.

Akiongea kwa njia ya simu toka nyumbani kwake Sintah baada ya mtandao huu kutaka kueleza anachukuliaje vitosho hivyo vya Shilole ambapo alisema" Kaka naambiwa sana na watu hasa wanaofatilia mitandao eti natafutwa kupigwa na Shilole sasa ninacho shangaa huyo Shilole anapafahamu kwangu aje basi anipige au kwenye ofisi zangu anapajua namkaribisha vizuri sana jamani" Alisema Sintah

Aidha Sintah aliongeza kusema kuwa" Mimi huwa sio mtu wa maneno yeye aje tu anipige na sio kutangaza kwenye mitandao kuwa ananitafuta anipige hayo mambo ya bifu siku hizi watu wanayachukulia upuuzi kutafuta pesa ndio mpango mzima hivyo mimi
namshauri Shilole kama underground wa sanaa nchini aachane na bifu badala yake akazane kwenye mambo yake ya kutafuta pesa kwa ajili ya maisha yake na familia kwani uzee unakuja" Alisema Sintah

PICHA YA LULU INSTAGRAM IMEWAACHA MIDOMO WAZI WANAWAKE WANAOSHINDWA KUTUMIA UBUFU KAMA WAKE WA KUINGIZA MKWANJA.

Chanzo cha ugomvi huo ulitokana na Sintah kuandika habari kwenye mtandao wake kuwa Shilole hawezi kuimba na Jennifer Lopez wa Marekani bora hata Linah wa THT anaweza kufanya hivyo kwa hiyo Shilole aache kuidanganya jamii.

Mtandao wa Sintah uliandika hivyo
Aidha Mashabiki mbalimbali hasa wasomaji wa kwenye mitandao wamemuunga mkono Sintah kuhusu kauri yake" Ni kweli jamani Shilole hawezi kuimba na Jennifer Lopez hayo ni masihara jamani kwenda marekani ndio aje kuongea ulojo kiasi hicho kwanza ikumbukwe kuwa wasanii wote wa tanzania kule Marekani hawajulikani hata, hasa kwa sisi tunaofatilia tunajia" Alisema mfanyabiasha wa kimataifa aliyejitambulishia kwa jina la Hamu Juma.


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA

INATISHA HII; KABURI LA MMOJA KATI YA WALIOPATA AJALI YA MUSOMA LAFUKULIWA NA WATU WASIOJULIKANA.

PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top