Wananchi mjini Musoma wakiwa eneo la makaburi ya Musima Bus kushuhudia tukio hilo.
LEneo la makaburi ya Musima Bus walipozikwa baadhi ya marehemu wa ajali ya mabasi ya Mwanza Coach na J4 Express iliyotokea wiki iliyopita.
UMATI wa watu jana umejitokeza katika makaburi yaliyopo jirani na stendi ya Musa Mabasi, mjini Musoma baada ya kubaini kuwa kaburi mojawapo kati ya yale waliyozikwa marehemu wa ajali ya mabasi ya Mwanza Coach na J4 Express wiki iliyopita limefukuliwa na mwili wa marehemu aliyejulikana kwa jina la Mzee Swai ukiwa nje na hauna baadhi ya viungo.
Baada ya kuwatawanya wananchi hao, polisi walifanya uchunguzi kisha kushirikiana na baadhi ya wananchi hao kuuzika tena mwili wa mzee Swai huku wakiahidi kufanya uchunguzi zaidi.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment