Ni taarifa ambayo imethibitishwa pia na kamanda Mpinga na kweli imehusisha gari la Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) saa kumi na moja alfajiri ambapo kifaru kimoja chenye tairi kwenye msafara wa jeshi hilo kimeripotiwa kuacha njia na kugonga nyumba.
Shuhuda alieongea na Power Breakfast ya CloudsFM amesema ‘Imetokea Mnolela kijijini Lindi kwenye msafara huu wa jeshi ilitangulia Iveco moja na nyuma vifaru viwili na walipofika kwenye eneo la shule kuna kona mbaya sana ambayo mara nyingi magari huwa yanaanguka kwahiyo kifaru kimoja kikakosa njia na kikagonga nyumba ya kwanza kikamkanyaga mwenye nyumba kikagonga nyumba ya pili kikazama kwenye hiyo sebule, kwa harakaharaka waliofariki ni watatu, Wanajeshi watatu na mwenye nyumba ya kwanza na wengine ni majeruhi wa hali mbaya kabisa’
‘Mmoja wa waliofariki ni mama mwenye nyumba ya kwanza ambae alikua amelala kwenye chumba cha mbele ndio alikanyagwa na kufariki papohapo, walioumia ni Wanajeshi waliokua wamekaa juu ya kifaru hicho, wamepelekwa kwenye hospital ya Mkoa wa Mtwara’ – Shuhuda
Bonyeza play kumsikiliza shuhuda wa ajali hii.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment