
Prizenta wa Star TV, Sauda Mwilima akiwa na mume wake.
Kikizungumza na Ijumaa Wikienda, chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Sauda, kilisema kwamba baada ya wawili hao kufunga ndoa, Kauli aliondoka kwenda nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ alikokuwa akifanya shughuli zake kabla ya kufunga ndoa na hadi leo hajawahi kurudi Tanzania.
“Yaani baada ya Sauda kufunga ndoa, mumewe alikaa kwa miezi michache hapa Bongo, nasikia hata tendo la ndoa walifanya mara mbili tu.
Angalia hapa Video Tamu na Mpya Kabisa ya Nicki Minaj ANAKONDA.
“Hata alipojifungua na mtoto kufariki dunia kwa bahati mbaya, mumewe hakuwepo na hadi leo hajarudi, ukweli inauma sana ila Sauda ni mvumilivu kwani ndoa yake ni shida,” kilisema chanzo hicho.Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wetu alimtafuta Sauda ambapo alikuwa na haya ya kusema:

Sauda Mwilima akivishwa pete na mume wake, Kauli Juma.
“Mimi siyo mtu wa kujionesha kwamba eti mume wangu yupo nchini hivyo akija huwa ni kimyakimya anakaa tunaendelea na mambo ya familia yetu basi muda ukiisha anaondoka na tulikubaliana tangu tukiwa wachumba hivyo ikitokea mmoja wetu ameamua kumfuata mwenzake na kwenda kuishi naye hakuna shida,” alisema Sauda.Sauda aliongeza kwamba ndoa yake iko vizuri na hawajaachana na endapo ingekuwa haipo asingevaa pete ya ndoa.

“Ndoa yangu haijavunjika, tuko vizuri na mume wangu japokuwa tuko mbali lakini kila mmoja anamwamini mwenzake,” alisema Sauda.
Wadau wanaifananisha ndoa hiyo na ya Aunt Ezekiel na kudai kuwa wawili hao hawachekani.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment