Monday, August 18, 2014

MKE WA MTU AMWAGIWA MAHARAGE YA MOTO, KISA NI MUME WA MTU.

My God! Mke wa mtu, Mwajuma Prima amelazwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro baada ya kumwagiwa mwilini sufuria la maharage yalitokuwa yakichemka jikoni, kisa kupeleka maneno ya umbeya kwa mume wa mtu.

Mke wa mtu, Mwajuma Prima akiwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.

Tukio hilo la kusikitisha lilijiri juzikati majira ya saa 12:00 jioni ambapo mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Fatuma ndiye anayehusishwa na msala huo uliotokea nyumbani kwake maeneo ya Mtaa wa Ndege, Msamvu mjini hapa.
JIONEE PICHA MBALIMBALI ZA BASI KUBWA JIJINI DAR MAARUFU KAMA CITY TRAIN LIKIKATIZA KARIAKOO.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walidai kwamba, siku ya tukio, Fatuma alimshutumu Mwajuma kuwa amekuwa akimwambia mumewe maneno ya umbeya ili kuwatenganisha.
“Huyu Mwajuma anaishi Kihonda, kila baada ya siku tatu anakuja kwenye nyumba hii kumsalimia mama yake mdogo.


Mama mdogo wa Mwajuma Prima akimuuguza mwanaye.

“Juzi Fatuma aligombana sana na mumewe na chanzo cha ugomvi huo ilidaiwa kuna mambo mwanaume huyo aliambiwa na Mwajuma.
“Mwajuma alipofika kwa mama yake mdogo ndipo Fatuma akamkwida na kumuuliza kwa nini alimwambia mumewe mambo ya umbeya?

“Mabishano yalishika kasi na mwishowe walipigana. Fatuma alipoona amezidiwa, akaingia jikoni na kuipua sufuria la maharage yaliyokuwa yakichemka na kumwagia Mwajuma mwilini,” alisema mmoja wa majirani aliyeomba hifadhi ya jina lake.

Mume wa Mwajuma Prima akiwa na mama mdogo wa mwajuma.

Akizungumza na gazeti hili, mama mdogo wa Mwajuma alisema: “Fatuma ni ndugu yetu, tunatoka naye kijiji kimoja Turiani. Ni kweli alimmwagia Mwajuma maharage ya moto mwilini.“Fatuma alikuwa anamshutumu mwanangu kumchonganisha na mumewe ndipo walipoanza kupigana.

“Fatuma alipoona kazidiwa aliingia jikoni akaipua sufuria la maharage yaliyokuwa yakichemka wna kummwagia mwanangu mwilini na kumsababishia majeraha makubwa.”
Mume wa Mwajuma, Peter Muhanda alikiri mkewe kupatwa na masaibu hayo na kwamba alitoa taarifa polisi ambapo mtuhumiwa alikamatwa.”
 


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU PICHA NA VIDEO ZA SHILOLE AKIWA MZIWANDA KITANDANI ZAVUJA MTANDAONI, JIONEE MWENYEWE HAPA.

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online