Tuesday, August 19, 2014

BABA AMUINGILIA BINTIYE KINYUME NA MAUMBILE.


Vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia bado vinaendelea Zanzibar baada ya watu wawili kushikiliwa na polisi kwa tuhuma za kubaka.

Katika tukio lililotokea Agosti 4, mwaka huu Muhammed Khafidh Thabit (50), anadaiwa kumbaka mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 14.

Mtuhumiwa huyo alimuingilia binti yake huyo kinyume na maumbile na kumsababishia madhara makubwa mwilini wake.

Akizungumzia kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mkadam Khamis Mkadam, alisema tukio hilo limetokea eneo la Misufini.

Alisema baada ya kuhojiwa mtoto huyo, alisema baba yake alikuwa akimlazimisha kufanya mapenzi baada ya mama yake kutengana na baba huyo.

Watch Video of Bill Gates wins the Ice Bucket Challenge with ridiculous machine.



Alisema uchunguzi wa kidaktari umeonesha kuwa mtoto huyo ameingiliwa mbele na nyuma.

Katika tukio lingine la mkoa wa Kusini Unguja  Polisi inamshikilia  Ali Hashim Ali (27) mkazi wa Mwera visiwani hapa kwa tuhuma za kumuingilia mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka tisa.

Kamanda wa polisi mkoani humo, Juma Said Khamis alisema kijana huyo alimrubuni mtoto huyo kwa kumuahidi kuwa atampatia mbuzi wa kufuga.

Alisema mtuhumiwa huyo alimchukua mtoto huyo na kumpeleka katika boma la nyumba na kumfanyia kitendo hicho cha kinyama.
Alisema mtuhumiwa ameshawahi kuwalawiti watoto wengine wawili wa kiume.

Watuhumiwa wote wapo chini ya ulinzi.
Akihutubia Baraza la Idi hivi karibuni, Dk Ali Muhammed Shein alikemea vitendo vya udhalilishaji na kutaka vipigwe vita.

Alisema takwimu za vitendo vya udhalilishaji zinaonesha kuendelea kuwepo kwa vitendo hivyo licha ya jitihada zinazochukuliwa na serikali na kushiriana na wanaharakati.
 
Credit: Nipashe


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

SEE HOW BROCK LESNAR DECIMATESS JOHN CENA TO CLAIM HE IS THE WWE WORLD HEAVYWEIGHT CHAMPIONSHIP.

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top