Wednesday, August 20, 2014

AUNTY LULU AKUMKUBALIA MPENZI WAKE WA ZAMANI YAISHE ILI AANZE UHONDO WA MAPENZI TENA!

BAADA ya kuachwa na mpenzi wake wa siku nyingi Bond, ambaye kwa sasa anadaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji wa filamu, Wastara Juma, Aunty Lulu amekubali yaishe na sasa hana tena kinyongo nao.

Mwigizaji wa filamu Bongo, 'Aunty Lulu'.

“Mimi sina tena kinyongo na Wastara, vile nilikuwa namfanyia tu vituko, lakini kwa sasa asiniogope wala asiwe na wasiwasi na mimi, nimeshaachana na Bond japokuwa tulitoka mbali sana na hakuna wanamke anayemjua kama mimi, siku ya harusi yao nitacheza mpaka asubuhi,”alisema Aunty Lulu.

Staa wa filamu Bongo, Wastara Juma akiwa na muigizaji mwenzake 'Bond'.

Msichana huyo aliyepata umaarufu baada ya kutwaa taji la Kimwana Twanga Pepeta, alitoa kauli hiyo hivi karibuni maeneo ya Kinondoni baada ya kutakiwa kutoa tamko juu ya uhusiano wa wawili hao, ambao awali alikuwa akiwatupia madongo na kuwapiga vijembe.

Alisema kwa sasa hana kinyongo na Wastara na amebariki uhusiano wao wa kimapenzi.




HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU (+18)DENTI WA CHUO AVUJISHIWA PICHA ZA UTUPU, BAADA YA KUJISAHAU NA KUMPA JAMAA FLASH YENYE GROUP WORK.

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top