Tuesday, July 22, 2014

MAOFISA WA MALAYSIA WAKABIDHIWA BLACK BOX NDEGE MH17 ILIYOLIPULIWA NA WAASI UKRAINE.

 Mwanajeshi wa wapiganaji wanaoiunga mkono Urusi akikabidhi mojawapo ya vifaa vya kutunza kumbukumbu (black boxes) vya ndege ya Malaysia MH17 iliyolipuliwa kwa maofisa wa Malaysia.
Vifaa viwili vya kutunza kumbukumbu (black boxes) vya ndege ya Malaysia vilivyokabidhiwa.


Mtaalamu wa Malaysia akikagua moja ya vifaa hivyo.

Vifaa hivyo vikiwekwa kwenye mfuko baada ya makabidhiano.

HATIMAYE wapiganaji wanaoiunga mkono Urusi wamekabidhi vifaa viwili vya kutunza kumbukumbu (black boxes) vya ndege MH17 ya Malaysia iliyolipuliwa kwa maofisa uchunguzi wa Malaysia huko Ukraine.

Makabidhiano hayo yamefanyika ikiwa ni baada ya wito mbalimbali kutolewa kuhusu maofisa wa uchunguzi kuruhusiwa kufanya uchunguzi wao eneo hilo la ajali iliyouwa watu 298.

Waziri  Mkuu wa Malaysia, Najib Razak ameeleza kuwa vifaa hivyo vilikabidhiwa mjini Donetsk jana baada ya mazungumzo ya muda mrefu na wapiganaji hao.


Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top