Wednesday, July 9, 2014

JOHARI ACHEKWA NA BONGO MOVIE KWA KUPORWA BWANA.

Msanii mkongwe wa filamu Bongo Blandina Chagula ‘Johari’
WASANII wa filamu Bongo, waliokuwa katika kamati maalum iliyoundwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ya kukabidhiwa ukamanda wa vijana, juzi walimcheka mwenzao, Blandina Chagula ‘Johari’ kwa kunyang’anywa bwana.

Tukio hilo lilitokea juzi maeneo ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam, ambapo wenzake walimcheka kutokana na aliyekuwa mpenziwe, Vicent Kigosi ‘Ray’ kuporwa na mwigizaji mwenzake, Chuchu Hans.


“Niachieni Johari wangu jamani, mnamkerakera kila wakati hadi anakosa amani kwani wanaume wameisha atapata mwingine” alisikika Steve Nyerere akimfariji msanii huyo mkongwe ambaye aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Ray.


Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top