Wednesday, July 23, 2014

BABY MADAHA NA SHILOLE WAFWATUANA.


Staa wa Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’.

MTIFUANO mzito umeibuka kati ya mastaa wa Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na Baby Madaha baada ya kurushiana vijembe.
Awali katika gazeti la Amani toleo la wiki iliyopita, Baby Madaha alinukuliwa akisema kuwa Mwezi wa Ramadhani unambana kiuchumi, kwa vile kumbi nyingi za starehe zimefungwa, hivyo anakosa shoo.


Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Shilole alisema anamshangaa Madaha kwa kukosa hofu ya Mungu, huku akimchana kuwa, haweki akiba, anaishi maisha ya kutegemea shoo ndiyo maana anaulalamikia mwezi huu.

Baby Madaha.

Madaha alivyoelezwa kuhusu maoni ya Shilole, alikuja juu na kutema cheche: “Shilole anatafuta kiki kupitia jina langu, kwanza si hadhi yangu. Siwezi kujibishana na msanii anayetegemea shoo za kwenye vigodoro, akatafute pa kutokea.”

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top