Tuesday, July 8, 2014

BABY MADAHA AENDA KWAO KUTAMBIKA ILI MAMBO YAKE YAENDE VIZURI.

MAKUBWA! Staa wa filamu na muziki Bongo, Baby Madaha anadaiwa kwenda kijijini kwao kutambika baada ya kuona mambo yake yanamwendea kombo.


Staa wa filamu na muziki Bongo, Baby Madaha.

Akizungumza na mwanahabari wetu, rafiki wa karibu wa Baby Madaha ambaye hakupenda kuanikwa, alisema kutokana na staa huyo kuona mambo hayaendi vizuri hasa kwenye muziki, ameamua kwenda nyumbani kwao Mwanza kwa ajili ya kutambikia mizimu ya kwao.

Baby Madaha.

Alipotafutwa Baby kuhusiana na ishu hiyo, alifunguka:
“Ni kweli niko nyumbani kwetu Mwanza, ni muda mrefu sijaja kumuona mama, kuhusu kutambika hilo ni lazima kwani nikiona mambo hayaendi vizuri, lazima niikumbuke mizimu ya kwetu,” alisema Baby.


Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top