Tuesday, July 22, 2014

8 MBARONI KWA KUTUPA VIUNGO VYA BINADAMU DAR.


Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akitoa taarifa kwa wanahabari.

JESHI la Polisi Kanda Maalum la Dar es Salaam linawashikilia watu nane na kuwahoji kuhusu tukio la kupatikana kwa viungo vya binadamu vilivyogundulika katika maeneo ya bonde la Mbweni Mpiji, Bunju B Julai 21, mwaka huu ambapo mifuko ya plastiki ipatayo 85 yenye mabaki ya viungo vya binadamu iligundulika.


Polisi walipata taarifa za tuki hilo kutoka kwa wasamaria wema.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, polisi walipofika eneo la tukio waligundua mifuko ipatayo 85 yenye viungo vya binadamu vilivyokaushwa na kukakamaa vikiwemo vichwa, miguu, mikono, mioyo, mapafu, vifua na mifupa ya aina mbalimbali ya binadamu.Katika eneo hilo, pia vilikutwa vifaa vinavyotumika hospitali kama vile mipira ya kuvaa mikononi (gloves) mifuko miwili iliyotumika, nguo maalum (apron) zipatazo 20 na karatasi mbili zenye maswali ya kujibu.

Baada ya tukio hilo, viungo hivyo vilichukuliwa na kupelekwa Hospitali ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.   

Wanahabari wakimsikiliza Kamishna Kova.

Baada ya uchunguzi wa kina imebainika kuwa viungo hivyo kwa mara ya mwisho vilikuwa katika Maabara ya Chuo Kikuu cha Madaktari IMTU jijini Dar na hivyo polisi wamewakamata na sasa wanaendelea kuwahoji watu nane ambao wanasadikiwa kuhusika na miili hiyo ikiwa ni pamoja na baadhi ya madaktari wa IMTU.

Jeshi la Polisi limesema litamuhusisha Mkemia Mkuu wa Serikali na hatimaye mara baada ya kukamilika uchunguzi, jalada litapelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua zaidi ili sheria ichukue mkondo wake.

Kamanda Kova amewaomba wananchi kuwa watulivu na wasiwe na wasiwasi wakati upelelezi ukiendelea.

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top