Mkali wa sinema za Kibongo, Wastara Juma.
Mkali wa sinema za Kibongo, Wastara Juma amepinga kitendo cha mastaa wa Bongo kuagwa Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar wanapokutwa na umauti.
Akizungumza na gazeti namba moja la habari za mastaa na kijamii Bongo, Ijumaa Wikienda juzikati, Wastara alieleza kwa huzuni kubwa kuwa hafurahii eneo la Leaders kutumika kuagia kwa sababu ni eneo hilohilo ambalo hutumiwa kwa starehe.
Wastara Juma akiwa katika moja ya msiba wa wasanii wa Bongo Muvi .
“Ukweli kwa upande wangu napinga mastaa kuagwa Leaders kwa sababu Leaders mara nyingi hutumika kama sehemu ya anasa. “Ningeiomba serikali itutafutie sehemu maalum kwa ajili ya kufanyia shughuli zote za misiba ya watu maarufu,” alisema Wastara.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment