Friday, June 13, 2014

LORI LATEKETEA KWA MOTO BAADA YA KUGONGANA NA LORI LINGINE HUKO IGURUSI MBEYA.

 
Lori la kusafirisha mafuta linateketea kwa moto.
Lori la kusafirisha mafuta likiwa na shehena kubwa ya mafuta aina ya Diesel limeteketea kwa moto baada ya kupata ajali ya kugongwa na lori lingine katika eneo la igurusi wilayani mbarali.
Ajali hiyo imetokea  ikihusisha lori lenye namba za usajili T417 ABF, mali ya kampuni ya Camel oil ambalo lilikuwa likisafirisha lita 35,000 za mafuta aina ya diesel kutoka jijini Dar es salaam kwenda nchini Congo DRC ambalo linadaiwa kugongwa na lori linguine. 
Baadhi ya wananchi ambao wameshuhudia ajali hiyo  wameitaka serikali kuwalazimisha wamiliki wa malori kuhakikisha magari yao yanakuwa na madereva wa akiba kwa kuwa wanaamini kuwa ajali hiyo imesababishwa na dereva wa lori moja wapo kusinzia wakati akiendesha gari kutokana na uchovu wa safari ndefu.


Ungependa stori kama hizi zisikupite na zikufikie wakati wowote? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza Like hapo juu

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top