Mwanadada kutoka tasnia ya filamu Bongo, Coletha Raymond ‘Koleta’ amesema kwamba suala la yeye kuolewa siyo la leo wala kesho na kwamba anakula ujana kwanza.
Mwanadada kutoka tasnia ya filamu Bongo, Coletha Raymond ‘Koleta’
Akipiga stori na paparazi wetu juzikati, Koleta alisema kwa sasa hafikirii kabisa suala la kuingia kwenye maisha ya ndoa kwa kuwa, kila jambo na muda wake na bado Mungu hajamuonesha mwanawume wa kweli, ni bora akaendelea kuwa ‘singo’.
“Kuolewa! Mmmh! Hapana kwanza, bado niponipo mpaka pale Mungu atakaponipa mwanaume sahihi wa kuwa naye. Ndoa kujipanga bwana, si kukurupuka tu, acha nile ujana kwanza,” alisema Koleta.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment