Wednesday, June 25, 2014

BATULI ARUDIANA NA MTUNISI.

Staa wa filamu Bongo Yobnesh Yusuph ‘Batuli’.
 WASANII wawili wa filamu, Nice Mohamed ‘Mtunisi’ na Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ ambao walikuwa wapenzi kabla ya kuachana na mwanaume huyo kuoa, sasa wamerudiana rasmi.

Kwa mujibu wa chanzo chetu kilicho jirani na wasanii hao kimesema wawili hao hivi sasa wanapika na kupakua.Kilisema baada ya kurudiana, kwa sasa wanaishi pamoja kama mume na mke maeneo ya Sinza, jijini Dar es Salaam huku wakiishi kwa amani na upendo.

“Yaani sasa hivi Batuli na Mtunisi wana mahaba niue kwani wanaishi pamoja wanaamka na kulala wote maeneo ya Sinza-Mawela lakini wanafanya kuwa ni siri yao, hawataki watu wajue,”kilisema chanzo hicho.
Hivi karibuni Batuli aliweka picha ya Mtunisi katika akaunti yake kwenye mtandao wa Instagram na kuandika maneno haya “Alichokipanga Mungu hakuna wa kukipangua.”

Nice Mohamed ‘Mtunisi’.

Alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, Batuli alisema hawezi kuzungumzia katika vyombo vya habari kwa vile mambo hayo ni maisha yake binafsi.

Kwa upande wake, Mtunisi alicheka na kudai kusikia kutoka kwa watu juu ya mwenzake kuweka picha yake mtandaoni na kuandika maneno ya kimahaba, kitu alichosema hawezi kuzuia nafsi ya mtu kumuweka moyoni.

Ungependa stori kama hizi zisikupite na zikufikie wakati wowote? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza Like hapo juu

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top