Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova akimkabidhi Askari wa usalama barabarani, Moses Alphage fedha taslimu Sh. milioni 2 zilizochangwa na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na wasikilizaji wa kituo cha Redio Clouds FM kupitia programu ya kuhamasisha na kupongeza utendaji kazi wa askari wa usalama barabarani jijini Dar es salaam iliyonedeshwa na kituo hicho cha Redio. Alphage huongoza magari katika daraja la Mlalakuwa, Kawe.

Askari wa usalama barabarani, Moses Alphage, akiondoka zake kwa mwendo wa kikakamavu mara baada ya kukabidhiwa cheti na pesa taslimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 2 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova (hayupo pichani).
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova (wa tatu toka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Askari wa usalama barabarani, Moses Alphage (wa pili kushoto) aliyeibuka kidedea kwenye programu ya kuhamasisha na kupongeza utendaji kazi wa askari wa usalama barabarani jijini Dar es salaam iliyonedeshwa na kituo hicho cha Redio na kujishindia Sh milioni 2. Wa kwanza kushoto ni Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Albert Maneno na kulia ni mtangazaji wa Clouds Said Mohamed maarufu Bonge.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment