
Lungi Maulanga.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mchongo huo ulifanyika kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram baada ya Shumileta anayesaka maisha nchini humo kuona picha ‘sex’ ya Lungi (iliyopo ukurasa wa nyuma), fasta akamtafutia mteja, raia wa Nigeria (jina kapuni).
Baada ya kumegewa mchapo huo, waandishi wetu waliingia mzigoni na kufanikiwa kunasa mawasiliano ya msanii wa filamu Bongo, Lungi Maulanga na Shumileta kupitia mtandao wa Instagram.

Staa wa filamu za kibongo Jennifer Mwaipaja ‘Shumileta’.
Lungi alipoulizwa na mapaparazi wetu juu ya mawasiliano hayo ya kibiashara alifunguka:
“Nyie mmepata wapi habari? Hiyo simu yangu ilipotea, nahisi mtakuwa mmeona mawasiliano yangu humo. Kwani Shumi kunitafutia bwana kuna tatizo gani? Bwana kaniona, kanipenda na mimi nimechati naye, kuhusu mambo ya kwenda Naigeria hiyo haiwahusu.”
Ili kuleta usawa wa habari, mapaparazi wetu walimtafuta Shumileta kwa njia ya simu, mambo yalikuwa hivi:
Mwandishi: Shumileta mambo vipi?
Shumileta: Safi, niambie.

Lungi Maulanga.
Mwandishi: Tumepata habari kuwa umemuuza Lungi kwa mwanaume Mnaigeria huko India?
Shumileta: Aliyekwambia nani? Mfuate muulize vizuri, mimi sizijui hizo habari.
Mwandishi: Mbona lakini kuna SMS zako zimefumwa kwenye simu ya Lungi ukimtafutia bwana?
Shumileta: Mfuate kamuulize mwenyewe.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment