Hii ni mara ya kwanza kwa Obama kukutana na papa Francis.
Rais Obama ameelezea furaha yake ya kukutana na papa mtu ambaye kulingana naye anaishi na kutenda kulingana na injili anayoihubiri.
Maswala mbali mbali yenye umuhimu wa kimataifa pamoja na kidini huenda yakajadiliwa katika mkutano huo.Wawili hao wanatarajiwa kujadili namna ya kupunguza tofauti iliyopo kati yao katika maswala mengi mbali na kujaribu kuinua maisha ya watu maskini duniani.
Papa Francis amekuwa mstari wa mbele akipigania kubadili sera na mtazamo wa Kanisa na viongozi duniani kuhusiana na mikakati ya kupunguza tofauti kubwa baina ya maskini na matajiri duniani .
Aidha viongozi hao wawili wanatazamiwa kujadili hali ilivyo Nchini Ukraine, na swala la upatikanaji wa amani mashariki ya kati. Mwafaka baina ya mitazamo tata ya wawili hao kuhusiana na maswala ya uavyaji mimba, matumizi ya dawa za kupanga uzazi na ndoa ya jinsia moja pia inatarajiwa kuwa kati ya mada itakayojadiliwa .
Baada ya kukutana na papa rais Obama ameratibiwa kukutana na rais wa Italia Giorgio Napolitano mbali na waziri wake mkuu Matteo Renzi.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment