Msanii wa filamu za Kibongo, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ amewapa
makavu laivu baadhi ya watu wanaoshangaa na kuhoji inakuwaje anatimiza
mwaka mmoja ndani ya ndoa bila kuzaa.
Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ akiwa na mumewe siku ya ndoa yao.
Akizungumzia maneno ambayo amekuwa akiyasikia kutoka hata kwa watu
wake wa karibu wakiwemo wasanii wenzake, Jack alisema anawashangaa kwa
kuwa wanashindwa kujua kwamba kuolewa ni sheria lakini kuzaa ni
majaliwa.
“Ni kweli ndoa yangu keshokutwa tu inatimiza mwaka mmoja lakini
nawashangaa wanaohoji kutokuzaa kwangu, wao wako nje ya ndoa hawajui
mambo yanaendaje, wakiingia watajua kuwa kuzaa ni majaliwa ya Mungu,”
alisema Jack.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment